Pages

Saturday, 10 August 2013

Fw: [AfricaWatch] L'armée de Tanzanie est prête à en découdre avec Kagame!



 
 

Tuesday, August 6, 2013

CHOKOCHOKO ZA RWANDA KWA... KAGAME KUKIONA

Na Mwandishi Wetu
CHOKOCHOKO zinazoendelezwa na Rais wa Rwanda, Paul Kagame dhidi ya Rais Jakaya Kikwete zimewakasirisha baadhi ya wananchi wakiwemo askari wa Tanzania na wakadai kuwa kiongozi huyo wa Rwanda atakiona cha moto akianza uchokozi
Rais Jakaya Kikwete.Wakizungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki iliyopita kwa sharti la kutoandikwa majina yao gazetini, baadhi ya askari walisema wanamshangaa Kagame kuitishia Tanzania wakati anajua kuwa hana ubavu wa kupigana nayo.
Askari wengi waliohojiwa, walisema Rwanda haina uzoefu wowote katika vita ya kimataifa ukilinganisha na Tanzania na Kagame akianzisha vita ni yeye atakayekufa kwa sababu vita haina macho.
"Kagame anajua kwamba Rais Kikwete si mgomvi na alimpa ushauri tu kwa kumwambia azungumze na waasi nchini mwake sasa kwa nini anaendelea kufanya chokochoko? Akianza vita itamuua. Kwa nini anamdhalilisha rais wetu?" alisema askari mmoja.
Rais wa Rwanda, Paul Kagame. Akaongeza: "Kagame amezoea vita ya wao kwa wao lakini Tanzania tumeshakwenda nchini Comoro ili kumng'oa Kanali Mohamed Bacar ambaye alikuwa aking'ang'ania madaraka katika Kisiwa cha Anjouan, tulipigana na Nduli Iddi Amin na akakimbia nchi, sembuse Kagame?" alihoji askari huyo.
Akaongeza: "Tumekwenda Msumbiji, Angola, Visiwa vya Shelisheli, Darfur na hata Lebanon, siyo kwa kuvamia bali kwa kuombwa na mataifa, hivyo Kagame aache kabisa kumkashifu rais wetu, amheshimu kama anavyoheshimiwa yeye."
Licha ya askari, wananchi mbalimbali waliohojiwa na gazeti hili, wamemshangaa Kagame kwa kumtusi Kikwete.
"Kwangu mimi nasema ni bora tukaachana na huu mpango wa Shirikisho la Afrika Mashariki kwa sababu dalili mbaya zinaonekana hata kabla ya kuungana," alisema Naomi Erasto, Mkazi wa Masaki, Dar.
http://magangaone.blogspot.ca/
__._,_.___
Reply via web post Reply to sender Reply to group Start a New Topic Messages in this topic (1)
Recent Activity:
---------------------------------------------------------- The Voice of the Poor, the Weak and Powerless. More News: http://theafricawatch.blogspot.co.uk/ ----------------------------------------------------------- Post message: AfricaWatch@yahoogroups.com Subscribe: AfricaWatch-subscribe@yahoogroups.com Unsubscribe: AfricaWatch-unsubscribe@yahoogroups.com List owner: AfricaWatch-owner@yahoogroups.com ----------------------------- Managed by Africa Social Media Group, London, UK
.
__,_._,___

No comments:

Post a Comment